Swahili ab initio paper 1 text booklet S...
Swahili_ab_initio_paper_1_text_booklet_SL_2010_May.pdf-pages/páginas M10/2/ANSWA/SP1/SWA/TZ0/XX/T Friday 21 May 2010
Showing 3-4 out of 5
Swahili ab initio paper 1 text booklet SL 2010 May...
Swahili_ab_initio_paper_1_text_booklet_SL_2010_May.pdf-pages/páginas M10/2/ANSWA/SP1/SWA/TZ0/XX/T Friday 21 May 2010
Swahili ab initio paper 1 text book...
Swahili_ab_initio_paper_1_text_booklet_SL_2010_May.pdf-pages/páginas M10/2/ANSWA/SP1/SWA/TZ0/XX/T Friday 21 May 2010
Page 3
2210-2841
–3–
Turn over / Tournez la page / Véase al dorso
M10/2/ANSWA/SP1/SWA/TZ0/XX/T
KIFUNGU B
UNGEPENDA KUSAFIRI KWENDA WAPI?
Tunafurahi kuwatangazia ratiba yetu ya safari za ndege kutoka Nairobi kwenda miji
mbalimbali duniani wakati wa kiangazi.
Huu ni wakati ambapo nauli ni za bei nafuu kuliko
wakati mwingine wowote, na ukiwahi kufanya buking utapata tiketi kwa urahisi sana.
Pia, kwa wale ambao wanasafiri mara kwa mara, watapewa punguzo (
reduction
) la nauli
pamoja na kulipiwa gharama za hoteli katika miji ambayo imewekewa alama ya nyota (*).
Punguzo hili si kwa mwaka mzima, ni wakati wa kiangazi tu.
Kuna punguzo maalumu pia
kwa watoto, wanafunzi, na wale ambao wanaenda fungate (
honeymoon
).
Karibu ufurahie
raha ya kusafiri katika ndege zetu kubwa na za kisasa.
Njoo upate ukarimu wa Kiafrika.
Usafiripo nasi utapumzika, hutachoka.
Kama upo Nairobi piga simu namba +254 722 009 007
tutakupatia ratiba yetu vizuri.
Ifuatayo ni ratiba ya safari za ndege za shirika letu.
Safari zote zinaanzia Nairobi.
K
UTOKA
N
AIROBI
K
WENDA
N
AULI
W
AKATI
W
A
B
EI
N
AFUU
M
ARA
N
GAPI
K
WA
S
IKU
/ W
IKI
T
AREHE
Z
A
K
UFANYA
B
UKING
T
AREHE
Z
A
K
USAFIRI
11 Jan – 13 Juni
01 Sept – 03 Des.
Addis Ababa
$760
Mara 4 kwa wiki
Machi 1 - Mei 30
Juni 10 – Sept
31
Atlanta
$1297
Siku 4 kwa wiki
Mei 1 – Juni 30
Julai 31 – Sept 30
Boston
$1191
Siku 5 kwa wiki
Mei 1 – Juni 30
Julai 31 – Sept 30
Cairo
$840
Siku 5 kwa wiki
Machi 20 – Mei 10
Mei 15 – Sept 30
Chicago
$1262
Siku 4 kwa wiki
Mei 1 – Juni 30
Julai 31 – Sept 30
Dakar
$1050
Siku 1 kwa wiki
Machi 20 – Mei 10
Mwezi wa Agosti tu
Dar es Salaam
$490
Mara 3 kila siku
Machi 20 – Mei 10
Mei 15 – Jan 15
Detroit
$1319
Siku 6 kwa wiki
Mei 1 – Juni 30
Julai 31 – Sept 30
London
$900
Siku 6 kwa wiki
Mei 1 – Juni 30
Julai 31 – Sept 30
Mombasa
$260
Mara 4 kila siku
Januari 1 – Apr 30
Mei 1 – Des 03
New York
$1191
Siku 6 kwa wiki
Mei 1 – Juni 30
Julai 31 – Sept 30
Kisumu
$200
Siku 2 kwa wiki
Mei 1 – Juni 30
Julai 31 – Sept 30
Washington (IAD)
$1268
Siku 7 kwa wiki
Mei 1 – Juni 30
Julai 31 – Sept 30
Zanzibar
$510
Mara 2 kila siku
Machi 20 – Mei 10
Mei 15 – Des 03
KARIBU UPANDE NDEGE NA SISI!
Imechotwa na kurekebishwa kidogo kutoka
http://
www.takimsholidays.com/flights/index.asp


Page 4
2210-2841
–4–
M10/2/ANSWA/SP1/SWA/TZ0/XX/T
KIFUNGU C
KISWAHILI AU KIINGEREZA KATIKA ELIMU?
Hayo hapo chini ni mawazo ya wanafunzi kuhusu lugha ya kufundishia katika elimu ya
sekondari na chuo kikuu.
Je, iwe ni Kiswahili au Kiingereza?
Abdul Taibar
Ninasoma shule ya sekondari.
Ninafikiri lugha zote mbili, Kiingereza na Kiswahili ni nzuri
kufundishia kwa sababu zote ni muhimu sana katika maisha yetu.
Josia Makaranga Elias
Ninasoma shule ya sekondari.
Kiingereza kinafaa kuendelea kuwa lugha ya kufundishia
sekondari na vyuoni. Wazazi wangu wanasema kuwa Kiingereza kitanisaidia katika maisha;
kwa mfano kitanisaidia kupata marafiki wengi kutoka nchi nyingine duniani ambao hawawezi
kuzungumza Kiswahili. Nitajua utamaduni wao na wao pia watajua utamaduni wangu.
Furaha Muselem
Waalimu watumie lugha zote mbili, Kiswahili na Kiingereza.
Hii itawasaidia wanafunzi
wote kwa sababu wale ambao walisoma shule ya msingi kwa Kiingereza sasa wataanza
kuelewa Kiswahili, na wale ambao walisoma shule ya msingi kwa Kiswahili sasa wataanza
kuelewa Kiingereza vizuri.
Tumpale Mwakalinga
Mimi nafikiri ni vizuri masomo yafundishwe kwa Kiingerza tu, na wanafunzi wote lazima
wajifunze Kiingereza vizuri sana.
Mimi sasa hivi ninasoma masomo yote katika shule ya
msingi kwa Kiingereza, na ninajua nitapata maisha mazuri sana baadaye.
Elizabeth Kiondo
Ninataka masomo yote katika sekondari na vyuoni yafundishwe kwa Kiswahili tu kwa sababu
ni lugha ya tangu utotoni, yaani ni lugha yetu ambayo tunaijua tangu tukiwa watoto. Pia wazazi
wetu wanaijua lugha hii kwa hiyo watatusaidia katika kazi za nyumbani (
homework
).
Wanafunzi
wengi
wanapata
shida
kuelewa
masomo
kwa
sababu
yanafundishwa
kwa
Kiingereza – lugha ya kigeni ambayo hawaielewi kabisa.
Kutoka
The Guardian, Jumapili
(Novemba 2008)


Ace your assessments! Get Better Grades
Browse thousands of Study Materials & Solutions from your Favorite Schools
International Baccalaurea...
International_Baccalaureate
School:
Swahili_ab_initio_SL
Course:
Great resource for chem class. Had all the past labs and assignments
Leland P.
Santa Clara University
Introducing Study Plan
Using AI Tools to Help you understand and remember your course concepts better and faster than any other resource.
Find the best videos to learn every concept in that course from Youtube and Tiktok without searching.
Save All Relavent Videos & Materials and access anytime and anywhere
Prepare Smart and Guarantee better grades

Students also viewed documents